John 12

Maria Ampaka Isa Mafuta Huko Bethania

(Mathayo 26:6-13; Marko 14:3-9)

1 aSiku sita kabla ya Pasaka, Isa alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Isa alikuwa anaishi. 2 bWakaandaa karamu kwa heshima ya Isa. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Isa. 3 cKisha Maria akachukua chupa ya painti moja
Painti moja ni kama nusu lita.
yenye manukato ya nardo
Nardo ni aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri.
safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Isa na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.

4 fNdipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Isa, akasema, 5“Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300
Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300.
na fedha hizo wakapewa maskini?”
6 hYuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.

7 iIsa akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu. 8 jMaskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.”

Shauri La Kumuua Lazaro

9 kUmati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Isa alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Isa, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Isa alikuwa amemfufua. 10 lKwa hiyo viongozi wa makuhani wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia, 11 mkwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake Wayahudi wengi walikuwa wanamwendea Isa na kumwamini.

Kuingia Kwa Isa Yerusalemu Kwa Ushindi

(Mathayo 21:1-11; Marko 1:1-11; Luka 19:28-40)

12 nSiku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Isa angekuja Yerusalemu. 13 oBasi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!”
Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.

“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”

“Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”

14 qIsa akamkuta mwana-punda akampanda, kama ilivyoandikwa,
15 r“Usiogope, Ewe binti Sayuni;
tazama, Mfalme wako anakuja,
amepanda mwana-punda!”

16 sWanafunzi wake Isa mwanzoni hawakuelewa mambo haya, lakini Isa alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye.

17 tWale waliokuwepo wakati Isa alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu, waliendelea kushuhudia. 18 uNi kwa sababu pia walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu ndiyo maana umati wa watu ukaenda kumlaki. 19 vHivyo Mafarisayo walipoona hayo wakaambiana, “Mnaona, hamwezi kufanya lolote. Angalieni, ulimwengu wote unamfuata yeye!”

Isa Anatabiri Kifo Chake

20 wBasi palikuwa Wayunani fulani miongoni mwa wale waliokuwa wamekwenda kuabudu wakati wa Sikukuu. 21 xHawa wakamjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakiwa na ombi. Wakamwambia, “Tungependa kumwona Isa.” 22Filipo akaenda akamweleza Andrea, nao wote wawili wakamwambia Isa.

23 yIsa akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa. 24 zAmin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi. 25 aaMtu yeyote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata kwa uzima wa milele. 26 abMtu yeyote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba yangu atamheshimu.

27 ac“Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe katika saa hii.’ Lakini ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu. 28 adBaba, litukuze jina lako.”

Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.”
29 aeUle umati wa watu uliokuwa mahali pale uliisikia nao ukasema, “Hiyo ni sauti ya radi,” wengine wakasema, “Malaika ameongea naye.”

30 afIsa akawaambia, “Sauti hii imesikika kwa faida yenu, wala si kwa faida yangu. 31 agSasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. 32 ahLakini mimi, nikiinuliwa kutoka nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.” 33 aiIsa aliyasema haya akionyesha ni kifo gani atakachokufa.

34 ajUle umati wa watu ukapiga kelele ukasema, “Tumesikia kutoka Torati kwamba ‘Al-Masihi
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
adumu milele,’ wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu?’ Huyu ‘Mwana wa Adamu ni nani?’ ”

35 alNdipo Isa akawaambia, “Bado kitambo kidogo nuru ingalipo pamoja nanyi. Enendeni maadamu mna nuru, msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui anakokwenda. 36 amWekeni tumaini lenu katika nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Isa aliondoka, akajificha wasimwone.

Wayahudi Waendelea Kutokuamini

37 anHata baada ya Isa kufanya miujiza hii yote mbele yao, bado hawakumwamini. 38 aoHili lilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema: “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu,
na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani?”

39 apKwa hivyo hawakuamini, kwa sababu Isaya anasema mahali pengine:
40 aq“Amewafanya vipofu,
na kuifanya mioyo yao kuwa migumu,
ili wasiweze kuona kwa macho yao,
wala kuelewa kwa mioyo yao,
wasije wakageuka nami nikawaponya.”

41 arIsaya alisema haya alipoona utukufu wa Isa na kunena habari zake.

42 asLakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi. 43 atWao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.

Amwaminiye Isa Hatabaki Gizani

44 auIsa akapaza sauti akasema, “Yeyote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali yeye aliyenituma. 45 avYeyote anionaye mimi, amemwona yeye aliyenituma. 46 awMimi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kwamba kila mtu aniaminiye asibaki gizani.

47 ax“Mimi simhukumu mtu yeyote anayesikia maneno yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa. 48 ayYuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho. 49 azKwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema. 50 baNami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lolote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.”
Copyright information for SwhKC